Pata taarifa kuu
ECOWAS- BURKINA FASO

ECOWAS kuendelea kuisadia Burkina Faso katika vita dhidi makundi ya kijihadi

Mwenyekiti wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, Umaro Sissoco Embalo ambaye pia ni rais Guinea Bissau, amesema jumuiya hiyo itaendelea kuisaidia Burkina Faso katika vita dhidi ya makundi ya kijihadi na kurejea kwa utawala wa kiraia.

Rais wa  Guinée-Bissau, Umaro Sissoco Embalo, ambaye pia ni mwenyekiti wa ECOWAS
Rais wa Guinée-Bissau, Umaro Sissoco Embalo, ambaye pia ni mwenyekiti wa ECOWAS © Nipah Dennis / AFP
Matangazo ya kibiashara

Embalo, alisema haya baada ya mkutano wake na kiongozi wa kijeshi wa taifa hilo Kapteni Ibrahim Traore, ambaye alisisitiza kuheshimu makubaliano na ECOWAS.

“Tutaangalia namna ya kuisaidia Burkina Faso katika yale ambayo taifa hili linahitaji mara moja.”amesisitiza Umaro Sissoco Embalo.

Ziara yake imekuja saa chache baada ya ile ya waziri wa maendeleo wa Ufaransa mjini Ouagadogou.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.