Pata taarifa kuu
KENYA- UHALIFU

Kenya: Maofisa wa polisi wanaswa wakijaribu kuwaibia raia

Kituo kimoja cha televisheni nchini Kenya kimesambaza picha za video zikiwaonyesha maofisa wanne wa polisi wanaodaiwa kujaribu kuwaibia watu wawili shilingi za Kenya milioni 2 ($16,000; £13,000) kwenye barabara moja jijini Nairobi.

Jiji la Nairobi
Jiji la Nairobi © Diaznash / Pixabay
Matangazo ya kibiashara

Waathirika waweroptiwa kuwa wafanyikazi katika duka la kubadilisha pesa ambapo walikuwa wametoa pesa kutoka benki iliyokuwa karibu.

Jaribio hilo la wizi liliripotiwa kuzimwa baada ya tahadhari kutolewa.

Maofisa hao wa Polisi walikamatwa baadaye baada ya wenzao kulinasa gari walilokuwa wakitumia kufanya uhalifu huo.

Wamefikishwa katika mahakama moja jijini Nairobi kwa makosa ya kujaribu kuwaibia raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.