Pata taarifa kuu
DRC- USALAMA

DRC: Waathirika wa vurugu za kasai bado wanatafuta haki

Msikilizaji ni miaka 6 sasa imepita tangu kutokea machafuko kwenye eneo la Kasai nchini DRC yaliyochochewa na wapiganaji wa kiongozi wa kijadi, Kamwina Nsapu, bado waathirika wa vurugu hizo wanatafuta haki.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya elfu 5 waliuawa kati ya mwaka 2016 na 2017, waathirika wakihoji mfumo wa mahakama za nchi hiyo katika kutenda haki.

Myrant Mulumba ni kiongozi wa jopo linalopigania haki za waathirika wa vurugu za kasai.

“Hivi leo tumeingia katika mwaka wa sita vyombo vya sheria nchini Congo vinaendelea kuzembea nasi tumeshtumu mara kadhaa swala hili.”amesema Myrant Mulumba.

Tangu wakati huo msikilizaji, familia zilizopoteza ndugu zao wamekuwa wakishinikiza mahakama ya ICC kuingilia kati upatikanaji wa haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.