Pata taarifa kuu
DRC- SIASA

LUCHA, Kuhamasisha raia kutomrejesha madarakani rais Tshisekedi nchini DRC

Vuguvugu la vijana wanaopigania maendeleo na demokrasia nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, LUCHA, limesema linapanga kufanya kampeni kuhamasisha raia kutomrejesha madarakani rais Felix Tshisekedi, wakimtuhumu kwa kushindwa kutimiza ahadi alizotoa wakati wa kampeni.

 Félix Tshisekedi rais wa DRC
Félix Tshisekedi rais wa DRC France24-RFI
Matangazo ya kibiashara

Miongozi mwa ahadi wanazodai rais Tschisekedi ameshindwa kuzitimiza ni pamoja na kudhibiti usalama mashariki mwa Congo, elimu bure na mazingira bora ya uchaguzi.

Bienvenu Matumo ni mmoja ya wanachama wa vuguvugu hilo jijini Kinshasa.

“Tunataka raia wachague watu ambao wako na malengo,watu ambao wanauwezo wa kubadilisha maisha yetu.” amesema Bienvenu Matumo

Rais Tschisekedi anatarajiwa kuwania kwa muhula wa pili katika uchaguzi ujao wa urais, uchaguzi unaofanyika wakati hali ya usalama ikiendelea kuwa mbaya katika eneo la mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.