Pata taarifa kuu
BURKINA FASO - USALAMA

Burkina Faso: Luteni Kanali Emmanuel Zoungrana, amerejeshwa jela

Nchini Burkina Faso, Luteni Kanali Emmanuel Zoungrana, amerejeshwa tena jela, baada ya kuwasilishwa tena kwenye Mahakama ya Kijeshi hapo jana, kwa tuhma za kuwa na njama ya kutaka kumpindua kiongozi was a sasa Kapteni Ibrahim Traoré.

Ibrahim Traoré, Kiongozi wa Kijeshi nchini Burkina Faso
Ibrahim Traoré, Kiongozi wa Kijeshi nchini Burkina Faso AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya afisa huyo wa jeshi kuachiwa kwa dhamana, wiki mbili zilizopita, baada ya kuzuiwa kwa miezi 11 jela.

Uongozi wa mashtaka kwenye Mahakama hiyo ya kijeshi, unasema Luteni Kanali Zoungrana, anakabiliwa na mashtaka mengine ya kuhatarisha usalama wa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Aidha, anashtakiwa kwa kushambulia makao makuu ya Shirika la Utanagazaji, gereza la kijeshi na makaazi ya kiongozi wa sasa Kapteni Traore kwa lengo la kumwondoa katika nafasi ya uongozi wa taifa hilo.

Mashtaka dhidi yake, hata hivyo, yanapingwa na Kanali Zoungrana, kupitia Wakili wake anasema si ya kweli bali ni ya kusingiziwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.