Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-USALAMA

Hatima ya wanajeshi 46 wa Côte d'Ivoire waliokamatwa nchini Mali kujulikana siku ya Alhamisi

Wanajeshi 46 wa Côte d'Ivoire wanaozuiliwa tangu Julai 10 nchini Mali wanatarajiwa kufikishwa mbele ya jaji leo Alhamisi Desemba 29.

Téné Birahima Ouattara, Waziri wa Ulinzi wa Côte d'Ivoire, anaongoza ujumbe wa serikali yake huko Bamako.
Téné Birahima Ouattara, Waziri wa Ulinzi wa Côte d'Ivoire, anaongoza ujumbe wa serikali yake huko Bamako. AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe rasmi wa Côte d'Ivoire ulikwendai Bamako siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita kufanya majadiliano juu ya wanajeshi 46 wa Côte d'Ivoire wanaozuiliwa nchini Mali tangu mwezi wa Julai, ambao wakuu wa nchi za Afrika Magharibi wametaka kuachiliwa kwao ifikapo Januari 1, kulingana na maafisa kadhaa nchini humo.

Mnamo Julai 10, wanajeshi 49 wa Côte d'Ivoire walikamatwa nchini Mali, wakielezewa kama "mamluki", kisha kushtakiwa katikati ya mwezi wa Agosti kwa "jaribio la hatarisha usalama wa taifa" na kufungwa jela.

Abidjan inahakikisha kwamba wanajeshi hao walikuwa kwenye misheni ya Umoja wa Mataifa, kama sehemu ya operesheni za msaada wa vifaa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) na kutaka kuachiliwa kwao, ombi lililoungwa mkono na wakuu wa nchi za Afrika Magharibi. Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) mnamo Desemba 4 huko Abuja, iliweka makataa hadi Januari 1 chini ya adhabu ya vikwazo vipya dhidi ya Mali.

"Ndugu zetu wa Côte d'Ivoire wamewasili. Ujumbe unaongozwa na Waziri wa nchi mwenye dhamana ya Ulinzi Téné Birahima Ouattara. Tutafanya kazi katika mazingira mazuri," waziri wa Mali aliliambia shirkala habari la AFP.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Togo Robert Dussey, ambaye nchi yake ni mpatanishi katika kesi hii, pia lizuru mjini Bamako siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.