Pata taarifa kuu

Senegal: Wabunge wawili wawekwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya vurugu bungeni

Nchini Senegal, wabunge wawili waliofanya vurugu dhidi ya mwenzao Amy Ndiaye kwenye makao makuu ya Bunge wako chini ya ulinzi wa polisi kwa shambulio la kukusudia na vitisho vya kifo. Wabunge hao ambao walikuwa watafutwa tangu Desemba 3, wamehojiwa na maafisa wa mahakama. Tangazo ambalo linakuja katika hali ya mvutano mkali wa kisiasa katika Bunge la kitaifa.

Picha hizo zilienea kwenye runinga na mitandao ya kijamii: katikati ya kikao, - Desemba 2, 2022 -, Mbunge Massata Samb wa chama cha PUR - chama cha muungano wa upinzani Yewwi Askan Wi - anamfuata kumshambulia Amy Ndiaye na kumpiga makofi.
Picha hizo zilienea kwenye runinga na mitandao ya kijamii: katikati ya kikao, - Desemba 2, 2022 -, Mbunge Massata Samb wa chama cha PUR - chama cha muungano wa upinzani Yewwi Askan Wi - anamfuata kumshambulia Amy Ndiaye na kumpiga makofi. © Dakaractu - AFPTV
Matangazo ya kibiashara

Massata Samb na Mamadou Niang ambao wamekuwa wakisakwa kwa siku kumi,  hatimaye walijiwasilisha kwa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai siku ya Jumanne, lakini walikaa kimya, kwa mujibu wa mawakili wao.

Mwishoni mwa mkutano huo, wabunge wawili wa chama cha upinzani cha PUR, mshirika wa muungano wa upinzani Yewwi Askan Wi, waliwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa "shambulio la kukusudia na vitisho vya kupigwa na vitisho vya kifo".

Baada ya ghasia hizi ambazo zilishangaza wengi nchini, Amy Ndiaye alielazwa hospitalini. Mbunge huyo alikuwa mjamzito kulingana na wenzake kutoka Benno Bokk Yakaar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.