Pata taarifa kuu
DRC- RWANDA-USALAMA

Rwanda: Wakimbizi raia wa Kongo wameandamana kwa madai ya kubaguliwa

Nchini Rwanda, wakimbizi kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waliandamana jana katika kambi yao ya Kigeme Kusini mwa nchi hiyo, kulalamikia kile wanachosema ni kubaguliwa kwa ndugu zao Mashariki mwa DRC, huku wakitaka kurejea katika nchi yao. 

Ramani ya nchi ya DRC
Ramani ya nchi ya DRC RFI/Anthony Terrade
Matangazo ya kibiashara

Kuishi ni haki yangu, ndivyo yalivyosomeka maandishi katika mabango kadhaa katika kambi ya Kigeme.

Solange ni mmoja wa waandamanaji anataka haki dhidi ya raia wa DRC wenye asili ya Rwanda. 

"Tunaandamana dhidi  ya mateso wanayoyapata Watutsi wanaoshi nchini DRC, hao ni ndudgu zetu.Siwezi kurudi huko kwa sabababu ya makundi kama FDLR, FARDC, Nyatura, Mai Mai ambao hawatutaki, wanatushambulia." 

Tunataka kurudi nyumbani, mamia ya waandamanaji kwenye kambi hiyo ya watu 15,000 walisikika wakisema mbele ya wanahabari wa Kimataifa.

Baadhi yao waliwasili nchini Rwanda mwaka 2012 kama Jacque, aliyekuwa Mwalimu huko Masisis mkoani, Kivu Kaskazini. 

"Tumechoka kukaa kambini, miaka 10 sasa, sina hata mbuzi.Nitaacha nini nyuma, nitakiachia nini kizazi changu" ? 

 Maandamano haya yanalenga kuonesha changamoto za raia hao wa DRC wenye asili ya Rwanda, wanaoishi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kama anavyoeleza Edson Munyakarambi, rais wa kambi hiyo ya Kigeme. 

"Bila shaka Jumuiya ya Kimataifa inatazama kinachoendelea nchini DRC na haisemi chochote.Tunataka haki, sio ya kuishi kambini, tuna haki kama watu wengine." 

Maandamano haya yamefanyika siku chache baada ya Ufaransa na Ubelgiji pamoja na Marekani, kuitaka Rwanda kuacha msaada wowote kwa waasi wa M 23, madai ambayo Rwanda imeendelea kukanusha. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.