Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Maandamano yanaendelea nchini Sudan licha ya makubaliano ya kutatua mgogoro

Mamia ya Wasudan wameandamana siku ya Jumanne kupinga makubaliano ya utatuzi wa mgogoro unaopaswa kuiondoa nchi katika mdororo ambao imetumbukia tangu mwaka jana, waandishi wa habari wa AFP wamebainisha.

Waandamanaji mjini Khartoum, Desemba 5, 2022.
Waandamanaji mjini Khartoum, Desemba 5, 2022. REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

"Hapana kwa mpango huo," umati wa watu umepiga kelele wakielekea ikulu ya rais huko Khartoum, nyumbani kwa mkuu wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, ambaye alichukua madaraka mwezi Oktoba 2021 na kuwatimua viongozi wa kiraia.

Mnamo Desemba 5, jeshi lililoko madarakani nchini Sudan, akiwemo Jenerali Burhane na kamanda wa kijeshi Mohamed Hamdan Daglo, walitia saini makubaliano ya mfumo na makundi kadhaa ya kiraia, ikiwa ni pamoja na Forces for Freedom and Change (FFC) ambayo wawakilishi wao walitimuliwa katika mapinduzi ya Oktoba 25, 2021.

Makubaliano haya, ambayo yanasalia kuwa ya jumla na kuweka makataa machache, yamekosolewa na wachambuzi na wanaharakati wanaounga mkono demokrasia ambao wanayaona kuwa "hayaeleweki" na "ya siyo faa" na kutilia shaka uwezo wake wa kutatua mkwamo wa kisiasa ambao nchi hiyo inashuhudia kwa miezi kumi na tatu.

Siku ya Jumanne, waandamanaji wameandamana mjini Khartoum wakiwa wamebeba mabango ya kudai haki kwa waliouawa wakati wa maandamano ya kuunga mkono demokrasia.

"Tunapinga makubaliano haya ambayo hayako wazi kuhusu madai yetu ya haki na uwajibikaji," Nisreen, muandamanaji mwenye umri wa miaka 38, ameliambia shirika la habari la AFP kutoka Khartoum. "Hatuna imani tena na jeshi. Tuliwapa imani yetu huko nyuma na walifanya mapinduzi".

Mapinduzi haya yaliharibu kipindi kigumu cha mpito kwa utawala wa kiraia, ambao ulianza baada ya kuondolewa madarakani mwaka 2019, chini ya shinikizo kutoka kwa jeshi na maandamano ya raia, dhidi ya rais wa zamani Omar el-Bashir, aliyekuwa madarakani kwa takriban miongo mitatu na sasa yuko jela.

Tangu wakati huo, karibu maandamano ya kila wiki dhidi ya mapinduzi yamefanyika licha ya ukandamizaji ambao ulisababisha vifo vya watu 122 kulingana na madaktari, katika nchi hii maskini sana, iliyokumbwa na mgogoro wa kiuchumi na kuongezeka kwa ghasia kati ya makabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.