Pata taarifa kuu
KENYA- SIASA

Kenya imeadhimisha miaka 49 tangu kujipatia Uhuru kutoka kwa Uingereza

Nchini Kenya, rais William Ruto, wakati wa maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru siku ya Jumatatu, na kuahidi shughuli zote za serikali zitafanywa kwa njia ya kidigitali kuanza miezi kadhaa ijayo.

Rais wa Kenya William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Aidha, ameongeza kuwa serikali yake itajenga miundo mbinu imara ya mtandao wa Internet katika miji mbalimbali nchini humo ili kuwaruhusu wananchi kupata shughuli za serikali kwa urahisi.

"Tunalenga kuhamishia asilimia 85 ya huduma ambazo zinasalia za serikali katika Mfumo wa kidigitali ili kila mkenya, popote alipo hataitajika kuabiri basi kwenda kutafuta huduma za serikali ," amesema.

Ruto aliyeingia madarakani mwezi Septemba, amekuwa akisema analenga kuongoza nchi itakayotoa nafasi kubwa kwenye maendeleo ya miundo mbinu ya Internet ili kukuza zaidi uchumi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.