Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Mali: Wanajeshi wa Mali, Warusi na wawindaji wa Dozo watuhumiwa wizi mkubwa wa ng'ombe

Nchini Mali, operesheni za jeshi dhidi ya ugaidi zinaendelea, kama vile madai ya unyanyasaji na dhulma dhidi ya raia. Katika wiki za hivi karibuni, visa vipya vya wizi vimeripotiwa katika maeneo ya Mopti na Bandiagara hasa: wizi mkubwa wa ng'ombe. Wanajeshi wa Mali, wawindaji wa jadi wa Dozo wanaoandamana nao pamoja na Warusi wanaosaidia jeshi la Mali, wanahusishwa.

Wanajeshi wa Mali na wasaidizi wao kutoka Urusi na  wawindaji wa Dozo wanashtumiwa wizi wa ng'ombe nchini Mali.
Wanajeshi wa Mali na wasaidizi wao kutoka Urusi na wawindaji wa Dozo wanashtumiwa wizi wa ng'ombe nchini Mali. David Baché/RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika wilaya za Fakala, Sio, Pignari, Doucombo, Fatoma au hata Sofara, kwa wiki kadhaa, vyanzo vingi vya ndani vimekuwa vikionya kuhusu wizi mkubwa wa ng'ombe unaofanywa na jeshi la Mali na wasaidizi wake: wawindaji wa jadi wa Dozo na wapiganaji wa Kirusi. Warusi hawa wanaotajwa ni wakufunzi wa kawaida kulingana na Bamako lakini idadi kubwa ya nchi za Ulaya, Afrika au Amerika inawataja kuwa ni mamluki wa kundi la Wagner kutoka Urusi.

Kulingana na vyanzo hivi, wizi huu unakusanya ng'ombe elfu kadhaa, na kondoo na mbuzi.

Wizi wa ng'ombe sio jambo geni: wakati wowote operesheni za kupambana na ugaidi za jeshi la Mali zinakumbwa na shutuma za unyanyasaji, kama vile mauaji ya watu wengi, madai haya yanajumuisha uharibifu na wizi wa vito, samani, nafaka au wanyama.

Lakini sasa inaonekana kwamba baadhi ya oparesheni zina lengo kuu la kunyang'anya baadhi ya vijiji mifugo yao. Rasilimali muhimu kwa wakazi wa wafugaji. Wawakilishi wa jumuiya, vyama na watafiti, wote wa Mali, wanajiuliza: je, ni suala la watu wenye njaa wanaoshukiwa kushirikiana na wanajihadi? 

Mwishoni mwa mwezi Oktoba, wanajihadi wa Jnim, kundi linalotetea Uislamu na Waislamu, lenye uhusiano na Al-Qaeda, lilidai katika taarifa kwamba walipata ng'ombe walioibiwa na jeshi la Mali, FAMA, na wasaidizi wao wa Urusi huko Bogolo, karibu na Bandiagara. Jeshi la Mali,limebaini katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba lilipata ng'ombe 600 mnamo Novemba 10 "kutoka mikononi mwa magaidi" huko Somadougou, katika eneo la Mopti. Jeshi linabainisha kuwa lilizirudisha kwa wakazi wa kijiji hiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.