Pata taarifa kuu

Ethiopia: Misaada inaingia tu katika maeneo ya Tigray yanayoshikiliwa na serikali

Nchini Ethiopia, msaada wa matibabu na chakula umeanza kuwasili katika maeneo kadhaa ya jimbo la Tigray katika siku za hivi karibuni. Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na shirika la Mpango wa Chakula Duniani wamesafirisha tani kadhaa za vifaa vya dharura na watapanga uwasilishaji zaidi katika siku zijazo, kwani jimbo hilo limetengwa kwa mwezi uliopita. Lakini hii bado haitoshi kukabiliana na hali hiyo.

Hata hivyo, msaada huu hadi sasa umefika tu katika maeneo yanayokaliwa na jeshi la shirikisho. "Mtu asidanganywe", kinalaumu chanzo cha matibabu cha Tigray. hospitali za Mekele hazikupokea "chochote isipokuwa mirija na glavu".
Hata hivyo, msaada huu hadi sasa umefika tu katika maeneo yanayokaliwa na jeshi la shirikisho. "Mtu asidanganywe", kinalaumu chanzo cha matibabu cha Tigray. hospitali za Mekele hazikupokea "chochote isipokuwa mirija na glavu". © RFI/ Sébastien Németh
Matangazo ya kibiashara

Kufikia Jumanne, shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (ICRC) imetuma lori mbili kwa Mekele zikiwa zimesheheni tani 40 za vifaa vya matibabu: "dawa" ambazo zimesambazwa kwa vituo vichache vya afya katika eneo jirani, amesema msemaji wa shirika hilo. Misafara mingine inatarajiwa kuchukua njia hiyokatika wiki ijayo, kwa mujibu wa chanzo hicho, pamoja na safari ya kuelekea mji wa magharibi wa Shire, baada ya ndege kutua siku ya Jumatano.

Malori ya shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, pia yameanza kurejea Tigray: Jumatano, karibu na Mai Tsebri (Kaskazini-Magharibi), na Alhamisi huko Alamata (Kusini), yakiwa na tani 300 za ngano, maharagwe na mafuta, limeeleza shirika la Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, msaada huu hadi sasa umefika tu katika maeneo yanayokaliwa na jeshi la shirikisho. "Mtu asidanganywe", kinalaumu chanzo cha matibabu cha Tigray. hospitali za Mekele hazikupokea "chochote isipokuwa mirija na glavu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.