Pata taarifa kuu

Mapigano FARDC-M23: Mazungumzo kati ya DRC na Rwanda yaanza tena Luanda

Kinshasa na Kigali zilianza tena mazungumzo ya pande tatu ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Angola, DRC na Rwanda yliofanyika Jumamosi, Novemba 5, huko Luanda, Angola.

Marais wa Rwanda Paul Kagame, João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi wa DRC wakati wa mkutano wao wa pande tatu mjini Luanda, Julai 6, 2022, kuhusu mvutano mashariki mwa DRC.
Marais wa Rwanda Paul Kagame, João Lourenço wa Angola na Félix Tshisekedi wa DRC wakati wa mkutano wao wa pande tatu mjini Luanda, Julai 6, 2022, kuhusu mvutano mashariki mwa DRC. AFP - JORGE NSIMBA
Matangazo ya kibiashara

Kwa jitihada za rais wa Angola na rais wa sasa wa ICGLR, Joâo Lourenço, mkutano huu ulilenga kurejesha hali ya kuaminiana kati ya DRC na Rwanda, ambayo imedorora tangu kuzuka tena kwa ghasia mashariki mwa nchi hiyo na kuituhumu Rwanda kuunga mkono waasi wa M23 katika machafuko hayo.

Mwishoni mwa kikao hiki, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Angola, DRC na Rwanda walikubaliana kudumisha mazungumzo kati ya mamlaka ya Kinshasa na ile ya Kigali.

Walibaini kuwa hii ndiyo njia ya kutatua mzozo wa kisiasa kati ya nchi hizi mbili.

Mawaziri Téte Antonio, Christophe Lutundula na Vicent Biruta waliamua kuweka ratiba ili kuharakisha utekelezaji wa yale waliokubaliana mjini Luanda tarehe 6 Julai.

Waliomba kutumwa mara moja kwa Tume ya uchunguzi huko Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.

 Mazungumzo haya pia yalitazamiwa kufanyika kwa mikutano ya uratibu kati ya mchakato wa Luanda na mchakato wa Nairobi na kuomba upande upatanishi kufanya mawasiliano kwa ajili hiyo.

Rais Joao Lourenço aliteuliwa na Umoja wa Afrika kama mpatanishi, kwa nia ya kufufua mazungumzo kati ya pande hizo mbili na kupunguza mvutano katika kanda hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.