Pata taarifa kuu

Mchungaji akamatwa nchini DRC baada ya kumchinja mwanawe

Mchungaji wa kanisa ya kiinjilisti kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliyeshtumiwa kumchinja mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 21, amekamatwa na polisi kaskazini mwa Kongo-Brazzaville, duru za kuaminika zimesema siku ya Ijumaa.

Vikosi vya usalama vya Congo-Brazzaville huko Nfilou, wilaya ya mji mkuu Brazzaville, Juni 22, 2022.
Vikosi vya usalama vya Congo-Brazzaville huko Nfilou, wilaya ya mji mkuu Brazzaville, Juni 22, 2022. AFP - DESIREY MINKOH
Matangazo ya kibiashara

Mwanamume huyu, aliyewasilishwa kama Mchungaji Galako, "alimchinja mtoto wake, mwanafunzi wa shule ya upili mwenye umri wa miaka 21, Jumatano wiki hii. Kwa sasa anashikiliwa" huko Bétou kaskazini mwa Kongo, chanzo cha polisi kimeliambia shirika la habari la AFP.

Tukio hilo lilitokea katika kitongoji cha Bétou, kinachojulikana kwa ukarimu wake unaotolewa mara kwa mara kwa wakimbizi kutoka nchi jirani ya DRC na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliohojiwa na shirika la habari la AFP kwa njia ya simu, mchungaji huyo alimkata koromeo mwanawe kwa kisu baada ya "kusikia sauti ya Mungu ikimtaka atoe dhabihu kubwa ili awe shujaa". "Alipata usaidizi wa wanaume wawili, waumini wa kanisa lake, pia kutoka DRC, ambao pia wako mikononi mwa polisi," kimeongeza chanzo cha polisi.

Kwenye mitandao ya kijamii, picha zisizovumilika zinaonyesha mwili mwili wa kijanaukitapaka damu.

Wanafunzi wenzake wa mvulana aliyeuawa walitaka kuchukua haki mikononi mwao, lakini maafisa wa polisi waliingilia kati, na kusababisha makabiliano makali kulingana na mashahidi. Takriban watu wawili (mwanafunzi mwingine na muuza vinywaji) waliuawa na wengine tisa walipigwa risasi na kujeruhiwa, kulingana na polisi, ambayo inasema imefungua uchunguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.