Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

DRC: Kambi ya Rumangabo, yakabiliwa na mzozo wa kibinadamu

Nchini DRC, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, kundi la waasi la M23 linashikia mji wa mpaka wa Bunagana tangu Juni 2022. Kurejea kwa uasi huu, ulishindwa mwaka 2013, ambao ulisababisha watu wengi kuhama makazi yao.

Kambi ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao katikati mwa Rumangabo, huko Rutshuru, DRC, Oktoba 10, 2022.
Kambi ya watu waliolazimika kuyahama makazi yao katikati mwa Rumangabo, huko Rutshuru, DRC, Oktoba 10, 2022. © Paulina Zidi / RFI
Matangazo ya kibiashara

Makumi ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wamepata hifadhi katika vijiji jirani, kama vile Rumangabo. Kijiji kidogo ambapo hali ya kibinadamu ni mbaya leo.

Kwa muda wa miezi minne, Rumangabo hatambui tena kitovu cha kijiji chake. Kati ya shule na barabara, sasa zimerundikana makumi ya mahema kwa ajili ya watu waliokimbia makazi yao. Takriban kaya 4,000 zimepata hifadhi katika eneo hili, ambalo kwa kawaida huwa na familia 1,500 pekee.

Justin Koyomayombi, kiongozi wa eneo la Kisigari, anasema kijiji kina watu wengi: "Rumangabo ni kijiji kidogo na idadi ya watu imeongezeka karibu mara tano wakati ikiendelea kukabiliwa na matatizo mbalimbali, hususan matatizo ya vyoo, ukosefu wa maji safi, katika ngazi zote. "

Hali ngumu ya maisha

Angèle ni miongoni mwa watu hawa waliokimbia makazi yao. Alikimbia na familia yake yote na kwa miezi minne amekuwa akiishi katika kijiji hiki katika mazingira magumu:

Jana tulipata chakula kutoka kwa serikali, lakini ni kwa siku mbili tu. Tuna njaa kwa kweli sasa, tunahitaji amani ili tuweze kurudi majumbani mwetu, vijijini kwetu.

Pia kuna Jane ambaye hivi majuzi alijiunga na watu waliokimbia makazi yao Rumangabo. Ameeeleza kuhusu safari yake ndefu, ambayo ilianza alipokimbia kijiji chake karibu na Bunagana wakati wa mapigano kati ya jeshi na waasi wa kundi la M23. Mwanzoni, anasema kwamba alikimbia na familia yake hadi Uganda:

Tulikaa katika kambi ya muda kabla ya mamlaka ya Uganda kutuomba tuhamie mahali pengine pa wakimbizi. Lakini tulipendelea kurudi DRC na kwenda Rutshuru.

Kisha walijiunga na kambi kubwa zaidi ya watu waliohamishwa katika eneo hilo, ile ya Rwasa.

Lakini Jane anaeleza kwamba hali ya maisha huko ilikuwa ngumu sana. Yeye na watoto wake wawili waliugua na mtoto wake alipofariki, aliamua kuja Rumangabo kujaribu kumtibu binti yake.

Sasa anaishi peke yake na binti yake na anashiriki hema moja na familia nyingine ambayo tayari ilikuwa huko alipofika. Anamfikiria mume wake na watoto wake wengine waliobaki Rutshuru na hajui ni lini ataweza kuwaona tena.

Wingi huu wa watu bila shaka unalemea wakazi, hata kama Gentil Karabuka, kutoka mashirika ya kiraia, ahakikisha kuwa: mshikamano ni muhimu.

Sio wote waliohama wameweza kupata kimbilio shuleni au makanisani. Baadhi ya watu hawa waliohamishwa wanakaa na familia zinazowapokea.

Hali ambayo haiwezi kudumu, anasemaJustin Koyomayombi: “Hofu kubwa tuliyonayo hapa ni kwamba hali hii ikiendelea, tutajikuta tunazika watu. Hili linatuhuzunisha na kututia huruma kweli. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.