Pata taarifa kuu

Ujumbe wa ECOWAS kuhimiza utulivu baada ya mapinduzi nchini Burkina Faso

Ujumbe wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, ambao ulikuwa unatarajiwa kuzuru nchi ya Burkina Faso Jumatatu hii, hatimaye utakwenda nchini humo Jumanne wiki hii, kuhimiza utulivu baada ya kufanyika kwa mapinduzi mengine ya kijeshi wiki iliyopita. 

Ijumaa iliyopita, Kapteni Ibrahim Traore, mwenye umri wa miaka 34, aliongoza mapinduzi hayo, kwa kile alichodai Damiba alikuwa ameshindwa kukabiliana na utovu wa usalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi.
Ijumaa iliyopita, Kapteni Ibrahim Traore, mwenye umri wa miaka 34, aliongoza mapinduzi hayo, kwa kile alichodai Damiba alikuwa ameshindwa kukabiliana na utovu wa usalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii  inayoongozwa na Waziri wa Mambo ya nje wa Guinea-Bissau Suzi Carla Barbosa  na rais wa zamani wa Niger, Mahamadou Issoufou. 

Hatua hii inakuja baada ya kukubali kujiuzulu kwa Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba hapo jana , ambaye amekuwa madarakani tangu mwezi Januari, baada ya kumwondoa madarakani aliyekuwa rais, Roch Marc Christian Kaboré. 

Viongozi wa dini na wale wa kijamii wamesema Damiba alikubali kuachia madaraka ili kuepuka umwagaji damu, na ripoti zinasema amekimbilia nchini Togo. 

Ijumaa iliyopita, Kapteni Ibrahim Traore, mwenye umri wa miaka 34, aliongoza mapinduzi hayo, kwa kile alichodai Damiba alikuwa ameshindwa kukabiliana na utovu wa usalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi. 

Traore ameiambia RFI kuwa, ataheshimu mchakato wa kukabidhi madaraka kwa uongozi wa kiraia, ifikapo Julai 2024. 

Hali ya utulivu imeshuhudiwa lei katika jiji kuu Ouagadougou, baada ya siku mbili za makabiliano ya waandamanaji na maafisa wa usalama, nje ya ubalozi wa Ufaransa, kwa madai kuwa mkoloni huyo wa zamani alikuwa amempa hifadhi Damiba. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.