Pata taarifa kuu

Jeshi la Ukraine "limeingia" katika mji wa kimkakati wa Lyman, mkoa wa Donetsk

Jeshi la Ukraine limesema Jumamosi Oktoba 1 kwamba "limeingia" Lyman, mji wa kimkakati katika mkoa wa Donetsk (Mashariki), uliochukuliwa siku moja kabla na Moscow licha ya kulaaniwa na Kyiv na nchi za Magharibi. 

Barabara inayoelekea uwanja wa vita, karibu na eneo Lyman, Septemba 26, 2022.
Barabara inayoelekea uwanja wa vita, karibu na eneo Lyman, Septemba 26, 2022. © RFI/Anissa El Jabri
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Urusi limetangaza kwamba "limejiondoa" kutoka kwa jiji hili, ambalo lilikuwa limetumika kwa miezi kadhaa kamakambi ya askari na vifaa vya jeshi la Urusi.

"Vikosi vya Mashambulizi ya Anga vya Ukraine vinaingia Lyman, eneo la Donetsk," Wizara ya Ulinzi ya Ukraine imesema kwenye Twitter. Ujumbe unaoambatana na video ambapo wanaonekana wanajeshi wawili wakipeperusha bendera ya Ukraine karibu na bango la kuingilia Lyman.

Wakati huo huo, jeshi la Urusi limedai kujiondoa katika eneo hilo. "Wakitishiwa na kuzingirwa, wanajeshi wa Muungano wamejiondoa katika eneo la Lyman na kwenda kwenye eneo nzuri na salama zaidi," Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa.

Baada ya kuviteka tena vijiji vitano katika eneo hilo, msemaji wa jeshi la Ukraine upande wa mashariki, Serguiï Tcherevatiï, ametangaza kwenye televisheni, akinukuliwa na shirika la habari la Interfax-Ukraine, kwamba "takriban Warusi walio kati ya 5,000 na 5,500" walikuwa wamejijificha ndani na karibu na eneo la Lyman katika siku za hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Serguiï Gaïdaï, gavana wa eneo jirani la Lugansk, askari wa Kirusi waliopo "katika eneo hatari" la Lyman wana mambo matatu ya kufanya: kukimbia, kufa wote pamoja au kujisalimisha".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.