Pata taarifa kuu

Wimbi jipya la wahamiaji zaidi ya 600 waliofukuzwa nchini Algeria wawasili Niger

Zaidi ya wahamiaji 600 kutoka nchi kadhaa za kusini mwa jangwa la Sahara wamewasili kaskazini mwa Niger baada ya kurudishwa kutoka Algeria, mamlaka huko Niamey imeliambia shirika la habari la AFP. 

Wahamiaji kwenye mpaka kati ya Niger na Algeria, karibu na eneo la Assamaka.
Wahamiaji kwenye mpaka kati ya Niger na Algeria, karibu na eneo la Assamaka. Jerome Delay / ASSOCIATED PRESS
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hizo zimethibitishwa na Shirika la Uhamiaji Duniani, ambalo hata hivyo halikutoa takwimu. Hii ni mara ya pili mwezi huu kwa wimbi kama hilo la wahamiaji wa Kiafrika kurudishwa kutoka Algeria.

Kwa mujibu wa mamlaka ya Niger, walifika kwa miguu siku tatu zilizopita, huko Assamaka, mji wa Niger karibu na mpaka wa Algeria: wahamiaji 669 kutoka Afrika Magharibi na Afrika ya Kati walifukuzwa kutoka Algeria. Miongoni mwao wengi wao ni wanaume, lakini pia wanawake 14 na watoto 5. Wengi wao kutoka Mali na Guinea, lakini pia kutoka Burkina Faso, Senegal, Côte d'Ivoire, Gambia, Sudan... Mataifa kadhaa kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Shirika la Uhamiaji Duniani limethibitisha "kuwasili kwa wimbi hili la wahamiaji", bila kutaja idadi yao.Limependekeza kuwapa usaidizi, hasa kuwapokea katika kituo cha Assamakawale wanaotaka kurejea nyumbani kwa hiari.

Hii si mara ya kwanza kwa Algeria, ambayo haina utaratibu wa kutoa hifadhi, kuwarudisha nyuma wahamiaji. Lakini hili ni wimbi la pili la ukubwa huu chini ya mwezi mmoja nchini Niger. Juni mwaka jana, shirika lisilo la kiserikali la Madaktari Wasio na Mipaka lilishutumu "matendo ya kinyama" yaliyofanywa nchini Algeria kwa wahamiaji wa Afrika Magharibi wanaotaka kuingia Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.