Pata taarifa kuu

Senegal: Amadou Ba ateuliwa kuwa Waziri Mkuu

Hatimaye Senegal imempata waziri mkuu mpya . Amadou Ba ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu Jumamosi hii, Septemba 17. Ni Waziri wa zamani wa Uchumi na Fedha na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje. Muundo wa serikali mpya bado unasubiriwa.

Amadou Ba wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Dakar mnamo Februari 16, 2020 alipokuwa bado Waziri wa Mambo ya Nje.
Amadou Ba wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Dakar mnamo Februari 16, 2020 alipokuwa bado Waziri wa Mambo ya Nje. AFP - ANDREW CABALLERO-REYNOLDS
Matangazo ya kibiashara

Habari hiyo imetangazwa kwenye RTS, shirika la utangazaji la umma, ambalo limekuwa likirusha hewani kipindi chake maalum kwa karibu saa tatu. Amadou Ba, 61, ana wasifu wa kisiasa. Aliyekuwa Waziri wa Uchumi na Fedha kuanzia 2013 hadi 2019, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 2019 na 2020. Jina lake lilikuwa mojawapo ya yale yaliyosambaa mitandaoni katika miezi ya hivi karibuni kwa wadhifa huu wa Waziri Mkuu. Alipokelewa asubuhi na Mkuu wa Nchi Macky Sall katika ikulu ya rais.

Uteuzi kwenye wadhifa huo ulisubiriwa kwa karibu miezi kumi, tangu wadhifa huu wa Waziri Mkuu, uliofutwa na Mkuu wa Nchi mnamo mwezi Mei 2019, ulirejeshwa mnamo Desemba 2021. Lakini, alikuwa hajateuliwa mpakasasa.

Katika ujumbe kwa taifa Ijumaa jioni, Rais Macky Sall alihakikisha kwamba "gharama ya maisha, ajira kwa vijana, kodi ya juu itakuwa vipaumbele vya juu vya serikali mpya". Serikali mpya ambayo inatarajiwa kwa mara nyingine baada ya kutangazwa kwa uteuzi wa Amadou Ba kama Waziri Mkuu wa Senegal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.