Pata taarifa kuu

Wanajeshi watatu wa Umoja wa Mataifa wajeruhiwa katika shambulizi la bomu Mali

Walinda amani watatu wa Umoja wa Mataifa, wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wanasafiria kushambuliwa na kilipuzi, Kaskazini mwa Mali. 

Walinda amani wa MINUSMA wakishika doria mjini Timbuktu, Desemba 8, 2021.
Walinda amani wa MINUSMA wakishika doria mjini Timbuktu, Desemba 8, 2021. © FLORENT VERGNES/AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea jana, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja huo kwenye ukurasa wake wa Twitter. 

Tukio hilo lilitokea katika barabara ya kutoka Ber kwenda Timbuktu, lakini jeshi hilo la MINUSCO halijataja uraia wa wanajeshi waliojeruhiwa. 

Jeshi la MINUSMA, lilitumwa nchini Mali mwaka 2013 kwenda kusaidia kupambana na makundi ya kijihadi. 

Hii sio mara ya kwanza kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa kushambuliwa na hata kuuawa nchini Mali, na tangu mwaka 2013, wanajeshi 175 wameuawa baada ya kushambuliwa na wanajihadi. 

MINUSMA ndio jeshi kubwa la Umoja wa Mataifa na lina walinda usalama Elfu 17 wakiwemo, wanajeshi, Polisi, raia na watu wa kujitolea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.