Pata taarifa kuu

Cameroon: Sita wafariki baada ya shambulio katika eneo linalozungumza Kiingereza

Nchini Cameroon machafuko yameua zaidi ya watu 6,000 tangu mwisho wa mwaka 2016 na kuwalazimu zaidi ya watu milioni moja kutoroka makazi yao.

Vikosi vya usalama ikisambaratisha maandamano ya wanaharakati wanaotaka kujitenga kwa eneo lililoitwa Ambazonia.
Vikosi vya usalama ikisambaratisha maandamano ya wanaharakati wanaotaka kujitenga kwa eneo lililoitwa Ambazonia. AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu sita waliuawa siku ya Jumanne katika "shambulio" la basi lililofanywa na "magaidi" kusini-magharibi mwa Cameroon, eneo ambalo vita vya mauaji vinahusisha polisi na makundi yanayotaka kujitenga kwa maeneo yao ambayo yanazungumza Kiingereza, serikali ilitangaza Jumatano.

"Kundi la magaidi waliokuwa na silaha nzito (maneno ambayo hutumiwa na mamlaka kuwataja wanaozungumza Kiingereza wanaotaka kujitenga), walifyatua risasi dhidi ya basi moja" kutoka kampuni ya Golden Express iliyotoka Douala ikibeba abiria 14, wanawake saba na wanaume saba, amesema msemaji wa serikali René Emmanuel Sadi, Waziri wa Mawasiliano.

Amebaini kwamba shambulio hilo lilitokea katika wilaya ya Muyuka jimbo la Fako Kusini-Magharibi mwa nchi eneo linalozungumza Kiingereza kwenye sehemu inayounganisha mji mkuu wa mkoa wa Buea hadi Kumba, katika jimbo hilo.

"Watu sita wameuawa katika shambulio hili la kigaidi la kikatili na la kinyama, yaani mwanamke mmoja (...) na wanaume watano (...), pamoja na majeruhi wanane", ambao ni wanawake sita na wanaume wawili, ameongeza Bw Sadi.

"Serikali ya Jamhuri inalaani vikali shambulio hili na la kuchukiza linalofanywa dhidi ya raia wasio na hatia na magaidi ambao wamepoteza ubinadamu wote kwa lengo la kueneza ugaidi miongoni mwa watu," amesema.

"Shambulio kwenye basi lilitekelezwa na + Amba boys + (jina maarufu la watu wanaozungumza Kiingereza wanaotaka kujitenga) ambao wanataka kuzuia kuanza tena kwa shule," afisa kutoka shirika moja lisilo la kiseikali ambaye hakutaka jina lake  litajwe ameliambia shirika la habari la AFP.

Maeneo ya Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi yamekuwa yakikumbwa na machafuko kwa miaka mitano kufuatia mzozo kati ya makundi yenye silaha yanayodai uhuru wa jimbo wanaloita "Ambazonia" na vikosi vya usalama vilivyotumwa kwa idadi kubwa na utawala wa Rais Paul Biya, 89, ambaye anatawala Cameroon kwa mkono wa chuma kwa karibu miaka 40.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.