Pata taarifa kuu

Tunisia kuwa mwenyeji wa mkutano ujao wa Francophonie

Tunisia itakuwa mwenyeji wa mkutano ujao wa kilele wa Shirika la Kimataifa wa Francophonie (OIF) mwezi Novemba mjini Djerba. Na hii licha ya kusitasita kwa baadhi ya nchi kama Canada, tangu Rais wa Tunisia Kaïs Saïed achukue mamlaka kamili.

Rais wa zamani wa Tunisia Beji Caid Essebsi akiwa na Katibu Mkuu wa OIF Louise Mushikiwabo mnamo 2018 wakati wa mkutano huko Yerevan.
Rais wa zamani wa Tunisia Beji Caid Essebsi akiwa na Katibu Mkuu wa OIF Louise Mushikiwabo mnamo 2018 wakati wa mkutano huko Yerevan. © LUDOVIC MARIN/AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuahirishwa mara mbili mfululizo, mkutano wa 18 wa Francophonie utafanyika katika kisiwa cha Tunisia cha Djerba. Habari hizo zilithibitishwa Jumanne na chanzo kilicho karibu na jumuiya hiyo. "Kumekuwa na uvumi na maneneo mengi", kama uwezekano wa mkutano huo kufanyika katika nchi nyingine, chanzo hiki kimebaini, lakini "Tunisia imeendelea kuwekeza katika maandalizi, ili kuendeleza shughuli mbalimali ... Kulingana na habari zetu, ujumbe kutoka Shirika la Kimataifa wa Francophonie pia ulifika Jumanne, Septemba 6 huko Djerba, ili kujionea wenyewe hali ilivyo.

Kuahirishwa mara mbili

Mkutano huu wa 18 wa OIF umeahirishwa mara mbili. Mara ya kwanza, mwaka wa 2020 kutokana na janga la UVIKO-19 na mara ya pili mwaka wa 2021. Nchi wanachama zilieleza kwamba zilitaka "kuruhusu Tunisia [...] kuandaa mkutano huu muhimu katika mazingira mazuri zaidi. Nchi hiyo wakati huo ilikuwa imekumbwa na maandamano, kupinga kuimarishwa kwa mamlaka ya Rais Kaïs Saïed na kupinga, hasa, kusimamishwa kwa shughuli za Bunge la Kitaifa kwa kipindi kirefu.

Tangu wakati huo, Bunge limevunjwa na Katiba mpya inayotoa mamlaka makubwa kwa Mkuu wa Nchi imepitishwa. Nakala iliyoidhinishwa na zaidi ya 94% ya wapiga kura. Lakini kwa kura ya maoni iliyoitikiwa na karibu 30% ya wapiga kura, kulingana na takwimu rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.