Pata taarifa kuu

Assimi Goïta na Paul-Henri Damiba kukutana kwa mazungumzo mjini Bamako Jumamosi hii

Rais wa mpito wa Burkina Faso, Luteni-Kanali Paul-Henri Damiba atakutana Jumamosi mjini Bamako na mwenzake wa Mali, Kanali Assimi Goïta, kulingana na vyanzo rasmi.

Luteni Kanali Paul Henri Sandaogo Damiba kwenye televisheni ya taifa ya Burkina Faso, tarehe 27 Januari 2022.
Luteni Kanali Paul Henri Sandaogo Damiba kwenye televisheni ya taifa ya Burkina Faso, tarehe 27 Januari 2022. © RTB via AP
Matangazo ya kibiashara

"Rais wa Burkina Faso, Luteni-Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, atafanya ziara ya kirafiki na kiserikali nchini Mali siku ya Jumamosi, Septemba 3, 2022", kulingana na taarifa kutoka kwa Ikulu ya rais ya Burkina Faso.

Ni "ziara ya kirafiki na kikazi", ilisema taarifa hiyo. Hii ni safari ya kwanza nje ya nchi kwa Luteni Kanali Damiba tangu achukue mamlaka kufuatia mapinduzi ya Januari 24, 2022.

Kulingana na Ikulu ya rais ya Burkina Faso, "ziara hii ya Mkuu wa Nchi kwenye kingo za Mto Djoliba ni sehemu ya nia ya mamlaka mpya ya Burkina Faso kuimarisha uhusiano bora wa karne za zamani kuhusu ushirikiano uliopo kati ya Burkina Faso na Jamhuri ya Mali".

Viongozi hao wawili watapitia masuala yenye maslahi ya pamoja kwa nchi zao za mpakani, likiwemo suala la usalama katika ukanda wa Sahel.

Baada ya Bamako, Paul-Henri Damiba atasafiri hadi Abidjan, nchini Côte d'Ivoire, siku ya Jumatatu, ambako anatarajiwa kukutana na Rais wa Côte d'Ivoire Alassane Ouattara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.