Pata taarifa kuu

Mali: Wanajeshi 49 wa Côte d'Ivoire wanaotuhumiwa kuwa "mamluki" washtakiwa na kufungwa

Wanajeshi 49 wa Côte d'Ivoire waliozuiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja katika mji mkuu wa Mali,  Bamako, na kushutumiwa na jeshi lililo madarakani nchini Mali kwa kuwa "mamluki", madai ambayo Abidjan inakanusha, wameshtakiwa kwa "kujaribu kuhatarisha usalama wa taifa" na kufungwa, vyanzo kadhaa vya mahakama vimebaini Jumapili hii, Agosti 14. 

Kiongozi wa kijeshi wa Mali Kanali Assimi Goita.
Kiongozi wa kijeshi wa Mali Kanali Assimi Goita. AP - Baba Ahmed
Matangazo ya kibiashara

"Askari 49 wa Côte d'Ivoire wameshtakiwa siku ya Ijumaa kwa "jaribio la kuyumbisha usalama wa taifa" na kuwekwa chini ya hati ya kufungwa," chanzo cha mahakama cha Mali kinachofahamu suala hilo kimeliambia shirika la habari la AFP. Mshirika wa karibu wa mwendesha mashtaka amethibitisha habari hiyo kwa shirika la habari la AFP.

Abidjan inahakikisha kwamba wanajeshi hawa walikuwa kwenye misheni ya Umoja wa Mataifa, kama sehemu ya operesheni za usaidizi wa vifaa kwa Misheni ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) na inaomba wanajeshi hao waahiliwe. "Askari hao 49 wamefunguliwa mashtaka na kuwekwa chini ya hati ya kukamatwa kwa ''kuhatarisha usalama wa taifa'' na sababu zingine",  afisa wa wizara ya sheria amelidokezea shirika la habari la AFP. Mazungumzo yanaonekana kwa sasa kama njia ilinayopendekezwa kwa kuachiliwa kwa wanajeshi hawa 49 waliokamatwa Julai 10 walipowasili katika uwanja wa ndege wa Bamako.

Togo ina jukumu la mpatanishi kati ya Côte d'Ivoire na Mali, lakini mazungumzo ya awali mnamo Julai 28 huko Lomé hayakuruhusu hayakuzaa matunda yoyote. Kulingana na chanzo kilicho karibu na mazungumzo yaliyoanzishwa chini ya mwamvuli wa Togo, "mazungumzo hayo, hata hivyo yalikuwa yakiendelea, yamekwama kutokana na baadhi ya mambo, ambayo yanaweza kuelezea urejesho huu wa mahakama katika kesi hiyo". "Mahakama itaendelea na kazi yake, lakini mazungumzo pia yataendelea," ameongeza.

Kesi hii inaonyesha mvutano kati ya Mali na Côte d'Ivoire, inayotuhumiwa na Bamako kwa kuwahimiza washirika wake wa Afrika Magharibi kuimarisha vikwazo dhidi ya wanajeshi wa Mali ambao wamefanya mapinduzi mawili tangu 2020, vikwazo aambavyo viliondolewa mapema mwezi wa Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.