Pata taarifa kuu

Mwandishi wa habari wa Ufaransa Olivier Dubois ashikiliwa kwa mizi kumi na sita Mali

Imepita miezi 16 tangu kutekwa kwa mwanahabari wa Ufaransa Olivier Dubois na wanajihadi katika eneo la Gao, Kaskazini mwa Mali. Kila tarehe nane kila mwezi, RFI hutoa nafasi kwa familia yake, ili kutoa maneno ya faraja kwa Dubois, wakiwa na matumaini kuwa ataachiwa huru

Mwandishi wa habari wa Ufaransa Olivier Dubois huko Nioro, Mali mnamo Septemba 2020.
Mwandishi wa habari wa Ufaransa Olivier Dubois huko Nioro, Mali mnamo Septemba 2020. © MICHELE CATTANI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Déborah Al Hawi Al Masri mke wa Olivier Dubois mwanahabari wa Ufaransa anayeendelea kushikiliwa na wanajihadi Kaskazini mwa Mali, amempa faraja mumewe akimtaka kuwa nasuburi na uvumilivu, siku moja ataungana na familia yake.

Mali na Ufaransa zinabaini kwamba zinafanya kinachowezekana ili mwandishi huyu wa abari aweze kuachiliwa, lakini bado hazitoi maelezo yoyote juu ya hatua zilizochukuliwa katika mwelekeo huu. 

Wakati Olivier Dubois akisubiriwa kuachiliwa, RFI inatoa nafasi kwa familia ya Olivier Dubois kila tarehe 8 ya mwezi. Katika uthibitisho wa mwisho uliotolewa na watekaji wake, Olivier Dubois alieleza kuwa aliweza kusikia jumbe hizi, mahali alipo, na kwamba ni wazi zilikuwa na msaada mkubwa kwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.