Pata taarifa kuu

Mafuriko nchini Senegal yasababisha kifo cha mtu mmoja Dakar

Nchini Senegal, mafuriko makubwa yalitikisa nchi hiyo siku ya Ijumaa Agosti 5, na kuua mtu mmoja huko Dakar. Kwa zaidi ya milimita 126 za mvua ilinyesha katika mji mkuu, mpango wa idara ya misaada ya kitaifa (ORSEC) ulianzishwa.

Mafuriko katika mji wa Dakar kufuatia mvua kubwa, Agosti 5, 2022.
Mafuriko katika mji wa Dakar kufuatia mvua kubwa, Agosti 5, 2022. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Mtu mmoja alifariki siku ya Ijumaa, Agosti 5, kwenye eneo la magharibi la Dakar ambalo lilikumbwa na mafuriko mchana kutwa, kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani. Mtaro ulipatikana ukijaa maji, na kusomba magari kadhaa.

Barabara nyingi zilifurika na msongamano wa magari ulifunga jiji hadi jioni. Magari yalisombwa na maji, maduka yalifurika maji, nyumba zilimezwa na maji ... uharibifu na hasara uwalizopata ni nyingi.

Kukatika kwa umeme, kutokana na mafuriko ya mtandao wa usambazaji, pia kumeonekana katika wilaya kadhaa za Dakar, kama vile Darou Salam Grand, Arafat, Les Mamelles au Monument ya Renaissance, kulingana na kampuni ya umeme ya Senegal, (Senelec).

Sen'eau, kampuni inayosimamia uendeshaji na usambazaji wa maji ya kunywa, pia ilifahamisha kuwa mtambo wa uhakika B ulifungwa siku ya Ijumaa, mapema jioni, ili "kuzuia uharibifu wa mitambo na hatari za umeme".

Ikiwa mvua imesimama kwa sasa huko Dakar, dhoruba, radi na mvua zinatarajiwa mwishoni mwa juma.

Uharibifu mkubwa waripotiowa katika mji wa pwani wa Ngor

Sio tu katikati ya mji wa Dakar ambao imeathiriwa sana na mafuriko haya. Pikine, Guédiawaye lakini pia mji wa pwani wa Ngor, ambao kijiji chake cha kitamaduni kiliathiriwa hasa. Wengi walijikuta wamenaswa na maji yalipopanda.

"Kuna nyumba zimeanguka, mabomba yamefurika kila mahali, mitaa yote imejaa matope kwa sababu barabara hazijawekwa lami, " amesema Elhajd Oumar Seye, Diwani wa Manispaa ya Ngor, anayesimamia Mazingira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.