Pata taarifa kuu

DRC: Operesheni ya 'kukomesha uzururaji' yageuka kuwa ghasia Kolwezi

Operesheni ya polisi katika mji wa Kolwezi, kusini-mashariki mwa DRC, ilizua ghasia Jumatano Agosti 4g, hali ambayo imelaniwa na mashirika ya kiraia. 

Moja ya barabara katika mji wa madini wa Kolwezi.
Moja ya barabara katika mji wa madini wa Kolwezi. Flickr.com CC BY-NC 2.0 Baas van Abel
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya mkoa imeviagiza vikosi vya usalama kuwaondoa ombaomba, watoto wa mitaani (Shege) na wahalifu katika jiji hilo. Lakini kulingana na kiongozi wa shiŕika moja la kiŕaia katika jimbo la Lualaba, operesheni hii ya polisi imefanywa bila utaratibu wowote ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Chadrack Mukad'End Naw anaelezea matukio ya huzuni huko Kolwezi: akina mama wanalia na huku wengie wakipandwa na hasira. Kulingana na kiongoziwa shirika hilo katika jimbo la Lualaba, zaidi ya watu kumi na tano walifariki katika operesheni hii ya polisi.

Baadhi ya wahanga walifariki wakiwa kizuizini, kama vile Ennock Kahozi Yile Bindu, mfanyakazi mwenye umri wa miaka 28 katika kampuni ya Mboko, baba wa watoto watatu. Wengine waliuawa kwa kupigwa risasi na vyombo vya usalama. Mchana, watoto, vijana na watu wazima walikamatwa kikatili mitaani bila kuchunguzwa utambulisho wao, kisha kuingizwa kwenye magari ya polisi na kutupwa jela. Wengine walilazimishwa kuvaa sare za maafisa wa idara ya za usalama: ovaroli za bluu na buti za njano. Ni lazima waandikishwe kwa nguvu kwa kazi ya shambani katika mashamba ya mahindi ya Kaniama Kasese.

Idadi kamili ya waliokamatwa haikuwekwa wazi. Mashirika ya kiraia katika jimbo la Lualaba yanaomba kufanyika kwa uchunguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.