Pata taarifa kuu
MSUMBIJI- UFISADI

Msumbiji: Waziri wa zamani Maria Helena Taipo afungwa jela miaka 16

Waziri wa zamani nchini Msumbiji amefungwa jela miaka 16 kwa kuhusika na vitendo vya ufisadi.

Ramani ya nchi ya Msumbiji
Ramani ya nchi ya Msumbiji RFI
Matangazo ya kibiashara

Maria Helena Taipo, mwenye umri wa miaka 60, ambaye pia ni mwanchama wa chama tawala cha Frelimo party, alikuwa waziri wa kazi kati ya mwaka wa 2005 hadi 2014, alituhumiwa kwa kufuja pesa za serikali dola milioni 1.7

Anatuhumiwa kwa kutumia fedha hizo kujijengea nyumba pamoja na kutumia katika matumizi mengine ya kibnafsi.

Maofisa wengine wanane waliohusishwa na sakata hiyo wamefungwa jela kati ya miaka 12 hadi 16.

Wakili wa kiongozi huyo wa zamani Inacio Matsinhe amesmea kuwa mteja wake atakata rufa dhidi ya uwamuzi huo wa mahakama.

Msumbiji ingali inapitia kipindi kigumu cha kiuchumi baada ya kumbwa na sakata ya dola bilioni 2, sakata iliyotajwa kutumbukiza taifa hilo katika mzozo mbaya zaidi wa kicuhumi tangu kujipataia uhuru wake kutoka kwa Ureno miaka 40 iliyopita.

Taifa hilo limeorodheshwa kama mojawapo ya mataifa masikini zaidi duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.