Pata taarifa kuu
TANZANIA-AJALI YA BARABARANI

Tanzania: Watoto wanane wapoteza maisha katika ajali ya barabarani.

Watu kumi wakiwemo wanafunzi wanane wamedhibitishwa kufariki katika eneo la Mikindani katika mkoa wa Mtwara nchini Tanzania baada ya basi walimokuwa wakisafiria kupoteza mwelekeo na kuanguka.

Ramani ya nchi ya Tanzania
Ramani ya nchi ya Tanzania © https://wwwnc.cdc.gov/
Matangazo ya kibiashara

Japokuwa maofisa wa polisi hajawabini kilichosababisha ajali hiyo ya mapema leo, basi hilo linaaminika kuwa linamilikiwa na shule ya msingi King David huko Mikindani

Picha za mitandaoni zimewaonyesha maofisa wa uwokozi wakiwa katika la mkasa wakiwaokoa watoto waliojeruhiwa.

Katika taarifa yake Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kufuatia vifo vya watu 10 wakiwamo wanafunzi wanane vilivyosababishwa na ajali ya basi la shule.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ameeleza kusikitishwa na vifo vya wanafunzi 8 wa shule ya msingi ya King David na watu wawili wanaodhaniwa kuwa walimu wao vilivyotokea leo asubuhi huko Mtwara Mikindani baada ya gari la shule kuanguka kwenye shimo.

Rais Samia aidha amewatakia afueni ya haraka kwa wote waliojerhuiwa katika ajali hiyo wakati huu wanapoendelea kupokea matibabu.

Ajali za barabarani zimekuwa zikiongezeka katika mataifa ya Afrika katika siku za hivi punde. Wiki hii zaidi ya watu 30 wameripotiwa kufariki katika ajali nyengine ya barabarani nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.