Pata taarifa kuu
TANZANIA-AFYA

Tanzania: Watu watatu wafariki kutokana na ugonjwa usiojulikana.

Siku moja baada ya serikali ya Tanzania kuwatuma wataalam wa afya na wanasyansi kubaini chanzo cha ugonjwa usioeleweka wa watu kuvuja damu pauni kusini mwa Tanzania, watu watatu waripotiwa kufariki katika eneo la Lindi.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan © blog.ikulu.go.tz
Matangazo ya kibiashara

Watatu hao ni miongoni mwa watu 11 waliodhibitiswha kuwa ugonjwa huo ambao umezua hofu katika hilo la Afrika mashariki.

Akihutubua kikao cha 20 cha shirikisho la viongozi kanisa katoliki rais Samia alihusisha ugonjwa huo usiojulikana na athari zinazotokana na uharibifu wa mazingira.

Aidha rais alisema kuwa uharibifu wa mazingira umeathiri baadhi ya wanayama wa porini hali ambayo imewalazimu kukaribia binadamu hali inayoathiri afya ya binadamu.

Vifo hivyo vimedhibitishwa na afisa mtendaji wa afya nchini Tanzania, Aifelo Sichwale, wakati  akiwahutubia waandishi wa habari jijini Dodoma.

Wizara ya Afya pia imetangaza kuunda timu ya wataalam kutoka idara ya Magonjwa ya dharura na Majanga, Epidemiolojia, mwanakemia mkuu wa Serikali, Taasisi ya Utafiti (NIMR), Chuo kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Taasisi hizo zimeungana na timu ya Mkoa ikihusisha pia Idara ya mifungo ambapo wanatarajiwa kufanya kazi kwa pamoja kubaini chanzo cha ugonjwa huo wa ajabu.

Wagonjwa wawili waliokuwa wametengwa katika kituo cha Afya cha Mbekenyera, wamepona ambapo wameruhusiwa kuondoka hosipitalini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.