Pata taarifa kuu
Nigeria - Elimu

Nigeria: Kuwasajili wanafunzi waliotoroka Ukraine

Serikali ya Nigeria, imesema itawasajili wanafunzi raia wa taifa hilo waliokatiza masomo yao nchini Ukraine, kutokana na uvamizi wa Urusi, ili kuendelea na masomo yao katika vyuo vikuu vya taifa hilo.

Wafunzi nchini Nigeria
Wafunzi nchini Nigeria The Guardian Nigeria
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya nje ya Nigeria imesema juhudi zinaendelezwa za kuhakikisha wanafunzi hao wanaendelea na masomo yao katika vyuo vya serikali nchini humo.

Tayari serikali imetoa fumo za maombi kwa wale wote wanaotaka kujiunga na vyuo hivyo vya serikali kuomba nafasi ya kuendelea na masomo yao.

Maelfu ya wanafunzi wa Nigeria waliokuwa masomoni nchini Ukraine walikatiza masomo yao baada ya uvamizi wa Urusi mwezi februari mwaka huu.

Licha ya hatua ya serikali, wanafunzi hao wanakabiliwa na changamoto ya kuendelea na masomo yao, kutokana na mgomo wa wahadhiri ambao unaendelea nchini humo, wakishinikiza nyongeza ya mishara

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.