Pata taarifa kuu

Shirika la DNA latoa wito wa kukabiliana vilivyo na ubakaji dhidi ya wanawake

Shirika la DNA Afrika,linataka  mataifa ya Afrika kuwekeza zaidi katika utalaam na vituo vya uchunguzi wa vinasaba au DNA, kusaidia kukabiliana na visa vya uhalifu. 

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati ambayo hayana vituo hivyo, wakati huu wanawake na wasichana wakiendelea kubakwa na makundi ya waasi Mashariki mwa nchi hiyo.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati ambayo hayana vituo hivyo, wakati huu wanawake na wasichana wakiendelea kubakwa na makundi ya waasi Mashariki mwa nchi hiyo. JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uhaba na ukosefu wa vituo hivyo, umeendelea kusababisha wanawake na wasichana wanaobakwa katika mataifa ya Afrika kutopata haki.

 

 

” watu wanashtakiwa kwa makosa makubwa, yafaa tathmini ya usambejeni yao ichukuliwe, watu wengi wanatekeleza makosa ya uhalifu wakirejelea makosa hayo.  Haya yote ni muhumu kwa kukusanya DNA, lakini tunahitaji, serikali na idara ya mahakama kushughulikia hili na kubadilisha sera zake”  amesema Ashley Spence, mwanaharalati kutoka nchini Marekani ambaye yupo katika mstari wa mbele kupambana na ubakaji.

Stephen Fonseca, kutoka kamati ya kimataifa shirika la msalaba mwekundu anaeleza namna uchuguzi wa vina saba unavyosaidia kuwatambua watu waliopotea. 

Uchuguzi wa vina saba hutumika kutambua mabaki ya watu waliofariki, pia kutambua watu waliopotea, hapa Africa watu wengi sana wamepotea na kuaga na njia pekee ya kuwatambua ni kupitia Uchuguzi wa vina saba.

Mkurugezi wa shirika la DNA for Africa Vanessa Lynch, anasema pamoja na changamoto hizo barani Afrika, bado kuna tumaini. 

"Tuna matabibu wa kutosha, wataalamu wa tathimini ya usambejeni, hatuhitaji msaada kutoka nje ya Afrika, wako hapa, tunawatazama, sharti tujiamini ili kuendeleza utalaamu huu mbele", ameongeza Vanessa Lynch  

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati ambayo hayana vituo hivyo, wakati huu wanawake na wasichana wakiendelea kubakwa na makundi ya waasi Mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.