Pata taarifa kuu

Libya: ICC yatangaza kifo cha kamanda wa kijeshi na kusitishwa kwa kesi

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Jumatano ilitangaza kifo cha Mahmoud Mustafa Busayf al-Werfalli, kamanda wa kijeshi nchini Libya anayeshukiwa kwa uhalifu wa kivita, na kusitisha kesi dhidi yake. Mahakama imefunga rasmi kesi yake.

Mahakama ya ICC ilikuwa hati ya kukamatwa mwezi Agosti 2017 dhidi ya Mahmoud Al-Werfalli.
Mahakama ya ICC ilikuwa hati ya kukamatwa mwezi Agosti 2017 dhidi ya Mahmoud Al-Werfalli. ICC-CPI/AFP
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa mahakama hiyo, iliyoko Hague (Uholanzi), unakuja zaidi ya mwaka mmoja baada ya ripoti kwamba Werfalli aliuawa kwa kupigwa risasi ndani ya gari lake na watu wasiojulikana, mnamo mwezi Machi 2021 huko Benghazi.

Mwendesha mashtaka hakutoa cheti cha kifo, lakini taarifa za mashahidi, picha na habari zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinathibitisha hilo. Na majaji walizingatia kwamba kifo kimetangazwa na kuamua kusitisha kesi.

Mahmoud Mustafa Busayf al-Werfalli alikuwa kamanda wa Brigedi ya al-Saiqa, kikosi maalum cha kikosi chenye mfungamano na Jeshi la Marshal Khalifa Haftar. Hati mbili za kukamatwa zilizotolewa dhidi yake kwa ombi la mwendesha mashtaka wa uhalifu wa kivita katika eneo la Benghazi kati ya mwaka 2016 na 2018 zimeondolewa. Zilikuwa zimetolewa kutokana hasa na video kadhaa zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, zikimhusisha katika matukio saba. Inasemekana aliamuru kunyongwa kwa watu wasiopungua 33. Na mnamo Januari 2018, pia alidaiwa kuwaua watu kumi mbele ya msikiti wa Benghazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.