Pata taarifa kuu
AFRIKA-URUSI-UKRAINE

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Macky Sall kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin

Rais wa Senegal, Macky Sall, ambaye pia ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, amewasili jana usiku (Alhamisi) mjini Moscow na anasafiri leo (Ijumaa) kwenda Sochi kukutana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin. 

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika  Macky Sall kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin mjini  Sochi, Juni  3  2022.
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Macky Sall kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Sochi, Juni 3 2022. © Kremlin of Russia
Matangazo ya kibiashara

Katika ziara hiyo Macky Sall ameandamana na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat.

Huu ni mpango wa kwanza wa kidiplomasia wenye lengo kuu la kukomboa akiba ya nafaka na mbolea, ambayo kizuizi chake kinaathiri nchi za Kiafrika", pamoja na kupunguza mzozo wa Ukraine.

Urusi na Ukraine pekee zinauza nje asimillia 30% ya ngano inayouzwa duniani.

Bei ya nafaka barani Afrika, imepanda kwa sababu ya kudorora kwa mauzo ya nje kutoka Ukraine, na hivyo kuongeza athari za migogoro na mabadiliko ya hali ya hewa na kuzua hofu ya machafuko ya kijamii.

Rais Putin atampokea Rais wa Senegal, Macky Sall, katika makazi yake ya Bahari Nyeusi huko Sochi.

Kampeni ya kijeshi ya Moscow nchini Ukraine na msururu wa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Urusi vimetatiza usambazaji wa mbolea, ngano na bidhaa nyingine kutoka nchi zote mbili, na kupandisha bei ya chakula na mafuta, haswa katika mataifa yanayoendelea.

Senegal ni mojawapo ya nchi 35 ambazo hazikupiga kura katika azimio la Umoja wa Mataifa, "kudai kwamba Urusi ikome mara moja kutumia nguvu dhidi ya Ukraine". 

Azimio hili lilipitishwa mnamo Machi 2 na nchi 141 zilizounga mkono na 5 zilipinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.