DRC
Waasi wawaua watu 22 Wilayani Beni Mashariki mwa DRC
Nchini DRC, watu 22 wameuawa katika kijiji cha Beu Manyama Kilomita 40 Kaskazini Magharibi mwa Beni.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Cheza - 00:13
Matangazo ya kibiashara
Maafisa wa usalama, wanadai waasi wa ADF ndio waliohusika na mauaji hayo.
Kanali Charles Omeonga, ni kiongozi wa kijeshi katika Wilaya ya Beni amesema kinachofanywa na jeshi kuwalinda raia.
Mauaji yalitokea katika eneo la Beu, waasi walijificha katika eneo hilo, jeshi linaendelea kufukuzana na waasi kila wakati.
Kuendelea kwa mauaji ya raia yameendelea kushuhidiwa Wilaya Beni, licha ya kuwepo kwa uongozi wa jeshi na wanajeshi wa Uganda wanaopambana na waasi wa ADF.