Pata taarifa kuu
DRC-RWANDA

DRC yasitisha safari ya Shirika la ndege la Rwanda , yadai inawaunga mkono M 23

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imetangaza kuwa inasitisha ndege za Shirika la Rwanda, kutua nchini mwake na imemwita Balozi wa Kigali jijini Kinshasa, baada ya madai kuwa, inawaunga mkono waasu wa M 23.

Patrick Muyaya, msemaji wa serikali ya DRC
Patrick Muyaya, msemaji wa serikali ya DRC © Ministère de la communication et des médias de la RDC
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya DRC Patrick Muyaya amesema hatua hii imechukuliwa baada ya kikao cha juu cha Baraza la Ulinzi na kulitaja kundi la M 23 kuwa na likagaidi na kuliondoa kwenye mchakato wa mazungumzo ya Nairobi na kuishtumu Rwanda, kulisaidia, madai ambayo Kigali imekanusha.

Akijibu hatua ya serikali ya DRC kulitaja kundi la M 23 kuwa la kigaidi, msemaji wa kundi hilo, Willy Ngoma amesisistiza kuwa, wana mkataba na serikali ya Kinshasa, wanaotaka utekelezwe.

Mapigano kati ya wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23, ambayo yamekuwa yakiendelea wiki hii, yamesababisha watu zaidi ya Elfu 72 kuyakimbia, makwao kwa mujibu wa takwimu, zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.