Pata taarifa kuu
Burkina Faso - Usalama

Burkina Faso : Wanajeshi 11 wauawa baada ya kushambuliwa

Wanajeshi 11 wa Burkina Faso wameuawa baada ya kambi ya jeshi ya Madjoari, kushambuliwa jana, taarifa kutoka idara ya jeshi ikisema, wanajeshi wengine 20 wamejeruhiwa na wanaendelea kupokea matibabu.

Luteni kanali Paul Henri Sandaogo Damiba kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso
Luteni kanali Paul Henri Sandaogo Damiba kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso © RTB via AP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi pia limesema lilifanikiwa kuwaua wanajihadi 15, ambao walikuwa wanataoroka baada ya kutekeleza shambulizi hilo.

Hakuna kundi  limekiri kuhusika na shambulizi hilo.

Kanali Paul Henri Damiba, ambaye aliongoza mapinduzi ya serikali y arais Roch Kabore, ameahidi kulipa swala la usalama kipao mbele kwa kuwaajiri maafisa zaidi wa usalama, pamoja na kubuni kamati itayoshiriki mazungumzo na wanajihadi ili kumaliza mashambulizi nchini humo.

Burkina Faso imekuwa ikishuhudia mashambulizi kutoka kwa wanajihadi tangu mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.