Pata taarifa kuu
SOMALIA-BURUNDI-AU

Wanajeshi 10 wauawa baada ya kushambuliwa na Al Shabab

Jeshi nchini Burundi  limesema, wanajeshi wake 10  wanaohudumu chini ya mwavuli umoja wa Africa wa ATMIS, nchini Somalia, wameuawa baada ya magaidi wa Al Shabaab kuvamia kambi yao jijini Mogadishu eneo la Shabelle. 

Magari ya jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia.
Magari ya jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia. © REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka Ofisi ya msemaji wa jeshi nchini Burundi, imesema mbali na wanajeshi hao kuuawa, wengine zaidi ya 25 wamejeruhiwa, na wanaendelea kupokea matibabu.

Haya hivyo, kutokana na hali ya majeruhi, huenda idadi ya vifo ikaongezeka, wakati huu jeshi la Burundi nalo likisema limefanikiwa kuwauwa magaidi 20 wa Al Shabab.

Magaidi wa Al Shabab kwa upande wao, wanadai kuwa, wamewauwa wanajeshi 173 wa Burundi, madai ambayo hayajathibitishwa na jeshi la mpito la kulinda amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia, ATMIS.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, amesema tayari amezungumza na rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye na kumpa pole kwa kuuawa kwa wanajeshi wa nchi yake.

Mbali na Burundi, mataifa mengine yaliyotuma wanajeshi wake nchini Somalia, ni pamoja na Uganda, Kenya, Ethiopia na Djibouti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.