Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine vyasababiha kupanda kwa gharama ya maisha Afrika

Shirika la fedha duniani IMF linasema, kupanda kwa gharama ya vyakula katika nchi mbalimbali barani Afrika kumechangiwa na vita vinavyoendelea nchini Ukraine na kuonya kuwa, huenda hali hii ikasababisha maandamano ya wananchi.

Mapigano yanaendelea kati ya Urusi na Ukraine, huku vifo vingi vikiripotiwa katika maenero kadhaa.
Mapigano yanaendelea kati ya Urusi na Ukraine, huku vifo vingi vikiripotiwa katika maenero kadhaa. REUTERS - SERHII NUZHNENKO
Matangazo ya kibiashara

IMF inaonya kuwa mataifa mengi barani Afrika yameanza kushuhudia kuyumba kwa uchumu wa mataifa yao tangu mwaka uliopita,  na kusababisha kupanda kwa bei ya vyakula hasa ngano na mafuta. 

Hata hivyo, hali imekuwa mbaya kutoka na vita vinavyoendelea kushuhudiwa nchini Ukraine, hali ambayo IMF inaonya kuwa, iwapo hali iutaendelea kama ilivyo, kutakuwa na uhaba wa chakula, kuongeza umasikini, watu kupoteza ajira na hivyo kusababisha maandamano ya wananchi wa matafa mbalimbali dhidi ya serikali yao. 

Baadhi ya mataifa ambayo yanaathirika moja kwa moja na vita vya Ukriane kwa kutegemea uagizwaji wa ngano kutoka nchi hiyo na Urusi kwa asililia 85 ni pamoja na Tanzania, Côte d'Ivoire, Senegal na Msumbiji. 

Onyo hili linakuja baada ya  ukuaji wa pato la bara Afrika ambalo lilikuwa limeongezeka kwa asilimia 4.5 mwaka ulipita, sasa kushuka mpaka asilimia 3.8 mwaka 2022. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.