Pata taarifa kuu

Afrika yakabiliwa na ongezeko la visa vya Covid-19

Shirika la afya duniani linasema, bara la Afrika limeanza tena kushuhudia ongezeko la maambukizi ya Covid-19, kufuatia nchi ya Afrika Kusini wiki chache zilizopita, kuanza kushuhudia ongezeko la maambukizi.

Idadi ya watu wanaombukizwa virusi vya corona imeshavuka zaidi ya watu 6200 wanaombukizwa kila siku nchini Afrika Kusini.
Idadi ya watu wanaombukizwa virusi vya corona imeshavuka zaidi ya watu 6200 wanaombukizwa kila siku nchini Afrika Kusini. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Hali hii huenda ikasababisha kuwepo kwa mlipuko wa tano, wakati huu mataifa mengi ya Afrika yakilegeza masharti ya kupambana na maambukizi hayo na kuwahimiza watukupata chanjo. 

Kwa upande wake Wizara ya afya ya Afrika Kusini imesema maambukizi ya virusi vya Corona yanaongezeka kwa maalfu kila siku na kwamba nchi hiyo imo kwenye ukingo wa kukumbwa na wimbi la tano la maambukizi ya virusi vya corona.

Waziri wa afya Joe Phaahla amewaambia waandishi wa habari kuwa itachukua muda ili kuweza kuitathmini hali kwa ukamilifu. Hata hivyo tayari idadi ya watu wanaombukizwa virusi vya corona imeshavuka zaidi ya watu 6200 wanaombukizwa kila siku.

Wizara ya afya nchini Afrika Kusini imesema ilitarajia maambukizi ya Corona kuongezeka kutokana na kwamba nchi hiyo inaingia katika msimu wa baridi.

Waziri wa afya ameserma idadi ya watu wanaolazwa hospitalini imeanza kupanda lakini amesema jambo jema ni kwamba hospitali bado hazijaanza kulemewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.