Pata taarifa kuu
SUDAN-USALAMA

Darfur: Watu 160 wauawa katika ghasia

Takriban watu 160 wameuawa Jumapili (tarehe 24 Aprili) katika ghasia huko Darfur, eneo la magharibi mwa Sudan lililoharibiwa kwa miongo kadhaa na vita, amesema Adam Regal, msemaji wa Shirika la Uratibu Mkuu wa Wakimbizi na watu waliolazimika kuyahama makazi yao Darfur.

Takriban watu 300,000 walikufa na karibu milioni 2.5 kukimbia makazi yao katika miaka ya kwanza ya ghasia, kulingana na UUmoja wa Mataifa.
Takriban watu 300,000 walikufa na karibu milioni 2.5 kukimbia makazi yao katika miaka ya kwanza ya ghasia, kulingana na UUmoja wa Mataifa. AFP/Ashraf Shazly
Matangazo ya kibiashara

Vurugu hizo zilianza Krink, kilomita 80 kutoka El-Geneina, mji mkuu wa Darfur Magharibi, siku ya Ijumaa, siku ambayo watu wengine wanane waliuawa, amesema Adam Regal, msemaji wa Uratibu Mkuu wa Wakimbizi na Watu Waliokimbia Makwao huko Darfur. Kulingana na afisa huyu, idadi hiyo inaweza kuongezeka wakati kuna watu angalau 46 waliojeruhiwa. Mwananchi wa kabila la Massalit aliripoti kwamba aliona maiti kahaa katika vijiji kadhaa katika sekta ya Krink, wakati Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ikitaka mamlaka kuhakikisha usafiri salama wa majeruhi hadi hospitali katika eneo hilo.

Kulingana na shirika hili, ghasia zilianza wakati wapiganaji wenye silaha kutoka makabila ya Kiarabu waliposhambulia vijiji vya Massalit, kabila ndogo la watu kutoka jamii ya Kiafrika, kulipiza kisasi kifo cha watu wawili wa makabila yao Alhamisi. Video na picha zilizochapishwa mtandaoni zilionyesha nguzo za moshi mweusi ukifuka kutoka kwa nyumba na vile vile vipande vya udongo ulioungua ambapo vibanda vya kitamaduni vilivyochomwa moto. Ukweli wa picha hizi haukuweza kuthibitishwa na vyanzo vilivo huru.

Eneo hilo lilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwaka 2003 kati ya utawala wa Waarabu walio wengi na waasi kutoka makabila madogo wakikemea ubaguzi. Takriban watu 300,000 walikufa na karibu milioni 2.5 kukimbia makazi yao katika miaka ya kwanza ya ghasia, kulingana na UUmoja wa Mataifa. Sudan, ambayo iliondoka mwaka 2019 katika miaka 30 ya udikteta chini ya utawala wa Omar al-Bashir, imetumbukia katika mdororo wa kisiasa na kiuchumi tangu mapinduzi ya mwezi Oktoba. Mwishoni mwa mwaka, kulingana na Umoja wa Mataifa, Wasudan 20 kati ya milioni 45 watakabiliwa na uhaba wa chakula. Na walioathirika zaidi nchini humo, mojawapo ya maskini zaidi duniani, ni zaidi ya watu milioni 3.3 waliokimbia makazi yao, karibu wote wanaishi Darfur.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.