Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC: Wabunge kutoka Kaskazini na Mashariki wapendekeza kusitishwa kwa sheria ya kijeshi

Nchini DRC, wabunge wa kitaifa kutoka mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri wanazidi kuchukua msimamo dhidi ya sheria ya kijeshi inayotumika kwa sasa katika mikoa yao tangu mwezi Mei 2021.

Operesheni za pamoja kati ya FARDC (vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) na wanajeshi wa Uganda, mnamo Desemba 14, 2021, Kivu Kaskazini.
Operesheni za pamoja kati ya FARDC (vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) na wanajeshi wa Uganda, mnamo Desemba 14, 2021, Kivu Kaskazini. AFP - SEBASTIEN KITSA MUSAYI
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya kipekee ilichukuliwa na Rais Félix Tshisekedi kupambana na makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo.

Viongozi waliochaguliwa wanabainisha kuwa mauaji yanaendelea na hata hali kuwa mbaya zaidi inashuhudiwa. Waliwasilisha muswada jana ili kuomba kusitishwa kwa hatua hii katika mikoa yao. Wabunge hawa wafanya hivyo kulingana na vipengee vya katiba vinavyobainisha kuwa Bunge la kitaifa na Baraza la Seneti vinaweza kusitisha sheria ya kijeshi wakati wowote kwa kupitisha sheria.

Wabunge watano, waliochaguliwa kutoka maeneo ya Lubero, Butembo, Beni na Irumu, ndio watetezi wa muswada huu. Nakala iliyowasilisha katika baraza la mawaziri inapendekeza kusitishwa kwa utawala wa kijeshi katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri. Iwapo muswada huo utapigiwa kura na kutangazwa, mabunge ya majimbo na vyombo vya miko hiyo vilivyosimamishwa vitarejelea shughuli zao kama kawaida, kama vile mahakama za kiraia.

Badala ya sheriaya kijeshi, wabunge wanapendekeza hasa kuimarisha vikosi vya jeshi na huduma zingine za usalama, na kuwapa vifaa vya kutosha na vyenye ubora zaidi.

Thaddée Katembo, aliyechaguliwa kutoka Lubero, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, ni mmoja wa waandishi wa nakala hii. "Jeshi lina jukumu kuu la kulinda uadilifu wa kitaifa. Hii inaweza kutumika tu wakati wa hali ya kuzingirwa. Hili ni jukumu lake. Kabla, wakati na baada ya hali ya kuzingirwa, jeshi lazima liendeleze jukumu hili," alisema.

Wabunge hawa pia wanapendekeza kuendelea kwa hatua ya pamoja ya kijeshi inayoongozwa na majeshi ya Kongo na Uganda katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri. " Inafaa leo kuendelea kusimamia oparesheni bila kuwepo kwa hali ya kuzingirwa. Kuna uratibu wa shughuli za pamoja kati ya nchi hizo mbili. "

Kuwasilishwa kwa muswada huu kunakuja wiki moja baada ya ujumbe wa Waziri Mkuu katika mikoa husika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.