Pata taarifa kuu

Cameroon yatia saini makubaliano ya kijeshi na Urusi

Cameroon imehitimisha makubaliano ya kijeshi na Urusi. Mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili walitia saini kwenye makubaliano hayo siku nane zilizopita mjini Moscow.

Mwanajeshi wa Cameroon huko Yaoundé, mji mkuu wa Cameroon.
Mwanajeshi wa Cameroon huko Yaoundé, mji mkuu wa Cameroon. ASSOCIATED PRESS - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yanahusu hati ya kurasa 13, iliyoanzishwa, kwa upande wa Cameroon, na Waziri wa Ulinzi, Joseph Beti Assomo, na kwa Shirikisho la Urusi na mwenzake, Jenerali Sergei Choïgou.

Kimsingi na katika kifungu cha 2 cha waraka huu, nchi hizo mbili zinakubaliana kubadilishana maoni na taarifa katika masuala ya sera ya kimataifa ya ulinzi na usalama, maendeleo ya mahusiano katika uwanja wa mafunzo ya pamoja na askari, elimu ya kijeshi, dawa, topografia au hata hidrografia ya kijeshi.

Pia wamekubaliana juu ya kubadilishana uzoefu, ulinzi wa amani na mwingiliano katika operesheni za kusaidia amani chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.