Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA

Waziri Mkuu Bachagha azuiliwa kuingia Libya, usafirishaji wa mafuta wasitishwa

Waziri Mkuu wa Libya Fathi Bachagha, aliyeteuliwa na Bunge mwezi Februari mwaka jana kuongoza serikali, kwa mara nyingine ameshindwa kuingia Tripoli ambako anaishi Waziri Mkuu wa zamani, ambaye bado anatambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Waziri Mkuu wa Libya Fathi Bachagha aliteuliwa na bunge mwezi Februari mwaka jana kuongoza serikali.
Waziri Mkuu wa Libya Fathi Bachagha aliteuliwa na bunge mwezi Februari mwaka jana kuongoza serikali. khalil / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na kushindwa kusuluhisha suala la serikali mbili zilizopo, mvutano unaongezeka nchini Libya. Baada ya kukutana mjini Tunis na maafisa kadhaa wa kijeshi kutoka magharibi mwa nchi, Waziri Mkuu wa Libya Fathi Bachagha amejaribu kuingia Libya ili kuweza kufika Tripoli kupitia mpaka wa Tunisia, lakini amezuiwa na vikosi vinavyoitii serikali ya Abdelhamid Dbeibah.

Matokeo: usafirishaji wa mafuta nje ya nchi umesitishwa baada ya kufungwa kwa maeneo kadhaa ya mafuta na vituo vya kusini na mashariki mwa nchi, vinavyodhibitiwa na makundi ya kiraia yanayomuunga mkono Fathi Bachagha.

Mizozo ya kisiasa

Wanatumai, kwa kufanya hivyo, watakuwa wameweka shinikizo kwa jumuiya ya kimataifa kumtambua Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Bunge. Kwa upande wake, Waziri Mkuu anayemaliza muda wake ametuma wanajeshi wake ndani na nje ya mji mkuu, na kuweka vizuizi na kuta za mchanga. Kwa hili, alitegemea wanamgambo wenye silaha kali kutoka Misrata, Zaouiya na Zentan.

Hali ya sasa inawafanya wakaazi wa mji mkuu huo kuhofia makabiliano mapya licha ya ahadi za wakuu hao wawili wa serikali kutofanya vurugu ili kusuluhisha tofauti zao za kisiasa.

Abdelhamid Dbeibah amedhamiria kusalia madarakani na bado anakataa kuondoka wadhifa wake. Kuhusu Fathi Bachagha, anashikilia serikali inayoondoka madarakani kuwajibika kwa ongezeko lolote, na analaani "ufujaji wa pesa za umma na unyonyaji wa mali ya Libya kwa manufaa ya serikali haramu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.