Pata taarifa kuu

Washington "yatiwa wasiwasi" na shutuma za "maangamizi ya kikabila" Tigray

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema Ijumaa, Aprili 8, kuwa "ilikuwa na wasiwasi mkubwa" na ripoti kutoka kwa mashirika mawili makubwa zinazoripoti "maangamizi ya kikabila" katika eneo lenye vita la Tigray nchini Ethiopia.

Mwanajeshi wa serikali ya Ethiopia akipiga kambi kando ya barabara katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia, Mei 2021.
Mwanajeshi wa serikali ya Ethiopia akipiga kambi kando ya barabara katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia, Mei 2021. AP
Matangazo ya kibiashara

"Tunaendelea kuzihimiza pande zote kuchukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kumalizika kwa uhasama, ufikiaji huru na endelevu wa kibinadamu, uchunguzi wa wazi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na wahusika wote, na suluhisho la mazungumzo la mzozo nchini Ethiopia" , ilisisitizwa katika taarifamsemaji wa wizara ya mamabo ya nje ya Marekani, Ned Price.

Katika ripoti ya pamoja iliyotolewa Jumatano, Amnesty International na Human Rights Watch (HRW) wanasema raia wa Tigrayan wamekuwa walengwa wa "kampeni isiyokoma ya mauaji ya kikabila" katika eneo la magharibi mwa eneo hili la kaskazini mwa Ethiopia, ambako mzozo ulizuka kati waasi wa Tigray na wanajeshi wanaoiunga mkono serikali mnamo mezi wa Novemba 2020. "Mateso haya ya kikabila" -- ubakaji, mauaji, uporaji, kunyimwa msaada wa kibinadamu -- yalifanywa na vikosi vya usalama vya mkoa jirani wa Amhara, wanamgambo wa Amhara na wenyeji, utawala, mashirika ya kiraia yameshtumu.

Ukatili Uliofanywa na Mamlaka ya Amhara

Akikumbuksha "wasiwasi mkubwa" wa Marekani kuhusu "ripoti za mara kwa mara za ukatili wa kikabila unaofanywa na mamlaka ya Amhara magharibi mwa Tigray", Ned Price amesisitiza juu ya taarifa yake kwamba Washington "ina wasiwasi mkubwa na matokeo ya ripoti kuhusu tabia hizi ni sawa na maangamizi ya kikabila". "Jeshi letu halijausika na uhalifu kama inavyodaiwa katika ripoti," msemaji wa serikali ya mkoa wa Amhara ameliambia shirika la habari la AFP, na kuyaita matokeo hayo ya "uongo."

Marekani ilishutumu Machi 2021 "vitendo vya maangamizi ya kikabila" vilivyofanywa na vikosi vya Amhara huko Tigray Magharibi. Mgogoro huo, ambao kwa muda ulienea zaidi ya Tigray, ulmesababisha maelfu ya watu wakiuawa, umesababisha mamilioni ya watu wanakabiliwa na njaa na pande zote mbili zimetuhumiwa kwa ukatili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.