Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC: Jeshi larejesha kwenye himaya yake maeneo kadhaa kutoka mikononi mwa M23

Vikosi vya wanajeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) vimeanzisha tangu Jumanne, Aprili 5, mashambulizi ya dhidi ya ngome zinazokaliwa na kundi la waasi la M23 katika eneo la Rutshuru. Lengo ni kuwaangamiza waasi wa M23, kulingana na jeshi.

Askari wa FARDC katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Askari wa FARDC katika mkoa wa Kivu Kaskazini. AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Mapema Jumatano hii, Aprili 06, FARDC imetangaza kurejesha chini ya himaya yake vijiji vya Bugusa, Tchengerero, Cheya na Mbuzi.

Mashirika ya kiraia ya Rutshuru na Jomba yakinukuliwa na Radio OKAPI, yanadai kuwa jeshi limekuwa likirusha makombora kuelekea vijiji vya Runyoni na Chanzu tangu asubuhi ili kuwafurusha waasi wa M23 ambao wamekalia eneo hili la kimkakati kwa angalau wiki mbili.

Makombora yamesikika tangu mapema Jumatano katika eneo hili la bonde chini ya vilima.

Mashirika ya kiraia ya Rutshuru yanabaini kwamba waasi wa M23 walijiondoa kwanza bila mapigano katika maeneo ya Cheya, sehemu ya Tchengerero na mbele kidogo. Pande hizo mbili zilipambana vikali katika vijiji vya Mbuzi, Gasizi, Runyoni na Chanzu, huku wanajeshi wa nchi kavu wa FARDC wakisaidiwa na mashambulizi ya anga.

Wakati huo huo, eneo hili limesalia tupu tangu kuanza kwa mashambulizi ya M23. Wakazi wengi walikimbilia katikati ya Rutshuru na Busanza

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.