Pata taarifa kuu

Msumbiji Mashambulizi yasababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao

Mwezi Januari, watu elfu kumi na nne na mia mbili, walikimbia makwao kufuatia mashambulio zaidi, shirika la Save the Children limesema, huku likiongeza vurugu za kutisha zilishuhudiwa ambazo ni pamoja na watu kukatwa vichwa nyumbani kwao katika wilaya zote za kaskazini mwa mkoa wa Cabo Delgado. 

Mapambano ya mji wa Palma yalianza Machi 24 mwaka jana, na mwaka mmoja baadaye bado huduma za kibinadamu zinahitajika kwa kiasi kikubwa.
Mapambano ya mji wa Palma yalianza Machi 24 mwaka jana, na mwaka mmoja baadaye bado huduma za kibinadamu zinahitajika kwa kiasi kikubwa. AFP - ALFREDO ZUNIGA
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Februari, takriban watoto saba wakiwemo wasichana watatu na wavulana wanne, walitekwa nyara na wanaume waliokuwa wamejihami, shirika hilo likihofu baadhi ya watoto hawa wanapewa mafunzo ya kuwa waasi au kutumika kama wanawake. 

Mapambano ya mji wa Palma yalianza Machi 24 mwaka jana, na mwaka mmoja baadaye bado huduma za kibinadamu zinahitajika kwa kiasi kikubwa. 

Mkurugenzi wa shirika hilo nchini Msumbiji Brechtje van Lith, anasema, shirika hilo limerekodi taarifa za mauaji ya halaiki yaliyoshuhudiwa na watoto dhidi ya wazazi wao na majirani, hali ambayo imesababisha wasiwasi mkubwa katika maisha yao. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.