Pata taarifa kuu
DRC-HAKI

DRC: Kiongozi nambari mbili wa chama cha Joseph Kabila kufungwa jela miezi sita

Ferdinand Kambere, ambaye tayari amekaa zaidi ya miezi miwili katika gereza kuu la Makala huko Kinshasa, chini DRC, alikuwa amefunguliwa mashitaka kwa jaribio la mauaji ya mwenzake kutoka chama ch PPRD. Upande wa mashtaka ulikuwa umeomba hukumu ya kifo, lakini mahakama ilichagua kutoa hukumu nyepesi ambayo chama tawala cha zamani hata hivyo hakikuridhika nayo.

Jela la Makala,anako zuiliwa Ferdinand Kambere, kiongozi nambari mbili wa chama cha Joseph Kabila.
Jela la Makala,anako zuiliwa Ferdinand Kambere, kiongozi nambari mbili wa chama cha Joseph Kabila. AFP PHOTO / JUNIOR D. KANNAH
Matangazo ya kibiashara

Ferdinand Kambere bado atalazimika kukaa jela miezi mitatu na siku chache. Naibu katibu mkuu wa chama cha PPRD ametakiwa na mahakama kulipa fidia ya dola 10,000 na faini ya dola 2,500.

Emmanuel Ramazani Shadary, katibu mkuu wa chama cha PPRD, anazungumzia kesi ya kisiasa: "Uamuzi huu wa kimahakama kwetu haukubaliki, nimesema na narudia tena, ni kesi ya kisiasa dhidi ya upinzani, kesi ya kisiasa dhidi ya chama cha PPRD. kwa sababu kila mtu anajua kuwa Kambere hana hatia. Lengo la tawala nyingine ni kututisha, kutunyamazisha. »

Kwa upande wake anaona, Ferdinand Kambere lazima aachiwe huru: “Nimekuwa nikisema kwamba haki hapa kwa sasa inaminywa, mahakama inashinikizwa na tunaomba wananchi wasimame, wasiache. Tutachukua hatua na katika kesi ya ndugu yetu Kambere, jambo la kwanza tutakalofanya ni kuwaomba mawakili wa Kambere wakate rufaa. »

Ukweli ulifanyika mwishoni mwa mwaka jana katika mgahawa wa Gombe, Kinshasa. Mabishano yalimpinga Ferdinand Kambere kwa swahiba wake Ardant Kabambi ambaye alijeruhiwa vibaya kichwani kwa kuvunjika chupa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.