Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-USALAMA

Zaidi ya hamsini wauawa katika shambulio la kuvizia Magharibi mwa nchi ya Ethiopia

Watu 53 waliuawa Magharibi mwa nchi ya Ethiopia, baada ya watu wenye silaha kuvamia msafara wa magari uliokuwa umewababe raia katika jimbo la Benishangul-Gumuz. 

Ethiopia inaendelea kukumlb<a na zimwi la mauaji.
Ethiopia inaendelea kukumlb<a na zimwi la mauaji. AFP - EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Haki za Binadamu nchini Ethiopia, katika ripoti yake imesema shambulizi hilo lilitokea Machi 2, na lililotokea karibu na mji wa Metekel. 

Wanajeshi 20 na raia watatu, waliuawa katika shambulizi hilo la kushtukiza, ambalo pia wavamizi 30 walipoteza maisha. 

Siku iliyofuata, watu wengine 11 waliuawa akiwemo mwanamume mmoja, aliyeteketezwa kwa moto na maafisa wa usalama. 

Tume ya Haki za binadamu nchini humo imewashtumu wanajeshi kwa kulisimamisha basi na kuwashusha raia nane kutoka jimbo la Tigray na kuwashtumu kupanga mashambulizi hayo. 

Machafuko haya ya Benishangul-Gumuz, ni tofauti na yale yanayoendelea kushuhudiwa katika jimbo la Tigray, Kaskazini mwa nchi hiyo, eneo ambalo limeshuhudia machafuko kwa miezi 16 sasa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.