Pata taarifa kuu

Tume ya kupambana na rushwa yatoa ripoti mpya kuhusiana na ufisadi Afrika Kusini

Tume ya kupambana na rushwa, Zondo, imekuwa ikichunguza kwa muda wa miaka minne kuhusu na ufisadi chini ya uongozi wa Rais Jacob Zuma (2009 hadi 2018), unaoshukiwa kuwa kiini cha mfumo mkubwa wa ufisadi ambapo fedha za makampuni ya umma zilifujwa kwa manufaa ya maslahi ya watu binafsi.

Rais wa Afrika Kusini na kiongozi wa ANC Cyril Ramaphosa akizungumza katika mkutano wa maadhimisho ya chama mnamo Januari 8, 2022.
Rais wa Afrika Kusini na kiongozi wa ANC Cyril Ramaphosa akizungumza katika mkutano wa maadhimisho ya chama mnamo Januari 8, 2022. AFP - PHILL MAGAKOE
Matangazo ya kibiashara

Ripoti za awali zilionyesha jinsi baadhi ya watu walivyotajirika: ndugu wa Gupta hasa, wakihusishwa na Jacob Zuma. Katika sehemu hii mpya, Tume inaeleza jinsi chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC, kilinufaika pakubwa kutokana na usaidizi wa kifedha wa kampuni binafsi kwa kufanya kampeni.

Bosasa ilikuwa kampuni yenye malengo yote kwa serikali. Kampuni hii ya kibinafsi iliyofanya kazi kubwa kwa niaba ya serikali ya Afrika Kusini kwa kuitekelezea huduma mbalimbali, hasa katika magereza, kama kuhudumia chakula wafungwa. Huku Jacob Zuma akiwa madarakani, serikali ilifanya mikataba mikubwa na kampuni ya Bosasa ambayo kwa upande wake ilitoa rushwa kwa viongozi wa kisiasa.

Bosasa pia ilikuwa kampuni muhimu katika kufadhili kampeni za uchaguzi za chama cha ANC. Mkurugenzi wa zamani alishuhudia kwamba majengo ya Bosasa yalibadilishwa mara kadhaa kuwa makao makuu ya kampeni, kile walichokiita "chumba cha vita", ili kumchagua Jacob Zuma.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo mwaka jana, Cyril Ramaphosa, makamu wa rais wa ANC wakati huo, alikubali kitendo hicho na kuzungumzia "upotovu", bila hata hivyo kuhisi kuwajibika kwa hali hiyo. Kwa upande wake, Jacob Zuma anabaini kwamba ufichuzi huu wa uwongo "haustahili hata kuwekwa hadharani."

Kwa upande wa upinzani, ripoti hii inaonyesha jinsi gani rushwa imekithiri nchini Aafrika kusini. Chama cha Democratic Alliance (DA), kinaona ripoti hiyo kama "uthibitisho wa kutisha zaidi hadi sasa na kubaini kwamba chama cha ANC ni kundi la uhalifu uliopangwa na kujifanya chama cha kisiasa".

Tume ya Zondo iliyoundwa mwaka wa 2018, ilitoa ripoti yake ya kwanza Januari 2022. Ripoti hii mpya ni sehemu ya mwisho ya uchunguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.